Thursday, 25 August 2016

WANAFUNZI WA MASOMO YA UDAKTARI WAFUNDISHWA KUTENGENEZA TAULO ZA KIKE

 Katika mafunzo ya wakufunzi juu ya hedhi salama mradi unaofadhiliwa na ubalozi wa Marekani nchini Tanzania na kutekelezwa na Kampuni ya Kasole Secrets na Msichana Initiative ambapo shule nne katika wilaya ya moshi vijijini ni wanufaika wa mradi huu. Wanafunzi wa masomo ya udaktari nane kutoka chuo cha udaktari KCMC na walimu wanne wa afya kutoka katika shule nufaika,walihudhuria mafunzo ya hedhi salama kwa siku tatu, moja ya warsha iliyofanyika katika siku hizi tatu za mafunzo ni kutengeneza taulo za kike, chupi, mifagio na dawa za kusafishia chooni kwa kutumia rasilimali zinazopatikana katika mazingira yao, wakufunzi hawa wanatarajiwa kwenda kuwafundisha jumla ya wanafunzi 500 kwa muda wa wiki 12 katika shule walizopangiwa  
Mkufunzi Judith Mlay ambaye ni Mhandisi Msaidizi katika idara ya Utafiti- Tanzania Engineering and Manufacturing organisation aliongoza mafunzo haya ya vitendo.
 Judith Mlay akitoa ufafanuzi wa kina kwa swali lililoulizwa na Florence Lyimo, mmoja wa wadau wa hedhi salama.
 Bi Judith Mlay, akionyesha jinsi ya kutengeneza kamba kwa kutumia majani ya migomba, Bi Judith alifafanua kua kamba hizi zinaweza kutumiwa kama nyenzo muhimu ya kusaidia kufunika mapipa ya takataka yaliyotengenezwa kienyeji.

Wakufunzi wakiweka vipimo sawa tayari kwa kutengeneza taulo za kike
 Bi. Hyasintha Ntuyeko ( Mkurugenzi Kasole Secrets) akisaidia kikundi kingine cha wakufunzi kuweka vipimo sawa, tayari kwa kuanza zoezi la kutengeneza taulo za kike
 Kazi ya ushonaji wa taulo za kike ikianza rasmi katika kikundi kimojawapo
 Zoezi la utengenezaji taulo za kike, lilikua na hatua mbalimbali zenye kushughulisha akili na kufurahisha, jambo lililowafanya wakufunzi wa kiume kufurahia sana zoezi hilo na hata kujaribu kubuni design nyingine, zoezi hili lilitupa mbinu mpya kabisa ambayo tunaahidi kuitumia ili kuweza kuwapata wakufunzi wa kiume kwa wingi zaidi na tunaamini tutafikia kipindi ambacho itakua ni kawaida kabisa kwa neno pedi/taulo za kike kutamkwa hadhari na jinsia zote bila kuona aibu.
 Mkufunzi Judith Mlay akionyesha hatua ya kwanza ya taulo ya kike iliyotengenezwa katika zoezi aliloliendesha
 Bi Judith Mlay akielekeza hatua ya pili katika kutengeneza taulo hii ya kike

0 comments: