Thursday, 30 April 2015

MAANDALIZI YA SIKUKUU YA HEDHI DUNIANI NA CTN TV

 Kipindi hiki kilikua live na kilichukua masaa 3 ambapo wananchi  walipiga simu na kutuma meseji, ni kweli jamii yetu inahitaji msaada, changamoto zinazowakuta wanawake wakati wa hedhi zinaathiri jamii nzima, tushirikiane kwa upendo
 Vitabu hivi vimeandaliwa na Kasole Secrets na kuchapishwa kwa msaada wa JHM foundation, vitabu hivi vinatoa ujumbe mhususi kwa jamii nzima ya Tanzania, vikimtaka kila mmoja wetu kusimama katika nafasi yake, kila mmoja abebe jukumu lake ili tuweze kufikia malengo, hatuwezi kufikia malengo kama upande mmoja pekee ndo utabeba jukumu hilo
Mwanahabari Batuli wa CTN akihoji zaidi juu ya nia ya kua na sikukuu ya hedhi duniani, alitaka kusikia zaidi juu ya faida ya siku ya hedhi duniani na baadae kuwapelekea taarifa hizi Watanzania kupitia taarifa ya habari.

Tuesday, 28 April 2015

HERI YA SIKUKUU YA HEDHI WATANZANIA

Usisite kuzungumzia hedhi, kwani bila hedhi mimi na wewe tusingekuwepo duniani, na bila hedhi salama ni vigumu kwa mabinti zetu kufanikisha ndoto zao, tambua hedhi si jukumu la mwanamke peke yake bali letu sote

Monday, 27 April 2015

TUNAPOJIANDAA KUSHEHEREKEA SIKUKUU YA HEDHI DUNIANI, TUNAHITAJI KUONA TAASIS ZINAKARABATI MIUNDO MBINU YA VYOO

 Choo hiki ni mali ya taasis moja nyeti sana ya serikali, iliyopo jijini Dar-es-salaam-Posta
 Kama unavyoweza kuona hapo, hiki choo kinahifadhi uchafu, unapomwaga maji uchafu unarudi, na si kwamba hakitumiki, kinaendelea kutumika
 Huo ni mlango wa kuingilia kwenye hicho choo, ni mlango mzuri sana, ila yaliyopo ndani ni mtihani mkubwa
 Hiki choo pia ni mali ya taasisi nyingine kubwa sana, tena ni wadau wakubwa wa mambo muhimu, kipo maeneo ya posta
 Huo ndo mlango wao ulivyo, umetengenezwa kwa Aluminium vizuri tuu, lakini ni sawa tu na kusema choo hakina mlango
 Unapokua ndani ya hiki choo, hii ndo hali unayokutana nayo, nafikiri hapana mlango kabisa hapa
 Muonekano wa vyoo vyote viwili
Muonekano wa vyoo vyote, ni sawa na kusema tuu, hii taasisi haina vyoo.

Swali langu ni kwamba, kama Taasisi muhimu kama hizi, miundombinu ndo hii, je huko vijijini hali ipoje?
Taasisi hizi hazina sababu zozote za kua na vyoo kama hivi... tunapojiandaa kusherehekea sikukuu ya hedhi duniani, tunatarajia mabadiliko kuanzia ngazi ya familia, pia tunatarajia taasisi hizi kufanya marekebisho ya haraka kwenye vyoo vyao..
Ninawatakia maandalizi mema ya sikukuu ya hedhi duniani.



Thursday, 23 April 2015

WATANZANIA TUNAPOJIANDAA KUSHEHEREKEA SIKUKUU YA HEDHI DUNIANI, EMBU TUJITAHIDI KUKARABATI MIUNDO MBINU YETU




Sioni sababu yeyote ya msingi ya taasisi yoyote kushindwa kurudishia milango ya vyoo pale inapobomoka, sielewi mjenzi wa vyoo hivi alifikiria nini kujenga vyoo bila kuweka mabomba ya maji au kufanya utaratibu wowote ili mtumiaji wa choo hiki aweze kupata maji akiwa ndani ya choo, sababu ya vyoo hivi kua vichafu na vyenye harufu kali kiasi cha watumiaji kuvitumia wakiwa wameziba pua, siielewi pia ni kosa la nani,
Je watumiaji wa kike ambao watajikuta wapo katika mazingira ya namna hii, watavitumiaje vyoo hivi? Je wataendelea kubaki eneo la kazi? Je ufanisi wa kazi wa huyu mama/ binti utakua wa aina gani katika mazingira haya?
Cha kushangaza zaidi vyoo hivi vipo jijini dar-es-salaam, tena katika mitaa inayoaminika wakazi wake wanakipato cha juu ukilinganisha na mitaa mingine
Kama mjini hali ni hii, je huko vijijini....?

WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI YA BAJAVERO DAR WAPATA MAFUNZO JUU YA HEDHI SALAMA.

 Mratibu wa Mradi wa Afya wa Help Kids Edith Peter Mziray akiwasihi wanafunzi kuwa wasikivu wakati wa semina ya Hedhi salama

Mkurugenzi mtendaji wa Kasole Secrets Hyasintha Ntuyeko ambao pia ni waandaaji wa siku ya Hedhi Duniani kwa Tanzania akiwauliza wanafunzi wa Darasa la tano hadi la saba changamoto wazipatazo wakati wanapoingia katika siku zao na pia kuwaelimisha juu ya Hedhi salama. 
 Mwanafunzi wa Darasa la Tano Anitha Norbart (12) akiuliza swali kama ni sahihi kutumia Mdalasini wakati akiwa katika siku zake?
 Daktari Edna Kiogwe akitoa elimu juu ya umuhimu wa kujitambua wakati wakiwa katika Hedhi na njia mbadala za kujiweka sawa pindi wanapokuwa katika kipindi hicho
 Wanafunzi wakiwa wanafundishwa moja ya mazoezi wanayotakiwa kuyafanya na Daktari Edna Kiogwe pindi wanapokuwa katika Hedhi.
 Baadhi ya wanafunzi wa Darasa la Tano sita na saba wakiwa wanafurahia Jambo wakati wa mafunzo
 Baadhi ya wanafunzi wakifuatilia kwa Makini Semina Hiyo
 Mmoja wa wanafunzi wa shule ya Msingi ya Bajavero akipewa zawadi ya Glory Pads ikiwa ni sehemu ya kusherekea siku ya Hedhi Duniani.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Bujeviro zamani Wamato wakifurahia Pads za Glory walizopewa ikiwa ni ishara ya kusherehekea sikukuu ya Hedhi Duniani. **** Kuelekea Kilele cha siku ya Hedhi Duniani ambayo itakuwa tarehe 28.05.2015 Mtandao wa Hedhi salama www.hedhisalama.com umeendelea kutoa mafunzo juu ya Hedhi salama ikiwa ni pamoja na changamoto,Magonjwa na mambo mbalimbali ambayo yanamtokea mwanamke anapokuwa katika Hedhi pamoja na ushiriki wa wanaume katika kujua maswala ya hedhi katika shule ya msingi ya yatima ya watoto waishio katika mazingira magumu ya Bajavero. Akitoa mafunzo ya Semina hiyo Daktari Edna Kiogwe alieleza kuwa kuna haja ya vijana tangu wakiwa wadogo wakapata Elimu juu ya Hedhi ili wanapokuwa wasijeshtuka pindi hali hiyo inapo wajia. Alieleza juu ya umakini na ufaulu mashuleni kuwa Wasichana wengi huahirisha shughuli za kimasomo kama kuhudhuria vipindi mbalimbali vya masomo yao Aliongeza ili Binti apate kuendana na hali hii anatakiwa ajivunie na kufurahia kipindi chote anachokua hedhi, atambue kwamba kila mwanamke hupitia kipindi hicho na hata wenzake darasani huvipitia vipindi hivyo vya hedhi, si yeye peke yake anaeingia hedhi. Pia Dkt. Edna alisisitiza kuwa Wanaume na wavulana wanahitajika kuelimishwa juu ya hedhi, wengi wao hawajui chochote juu ya hedhi na hua wanadhani mwanamke peke yake ndo anapaswa kufahamu juu ya hedhi. "Tukiwaelimisha wanaume juu ya hedhi, watakua msaada mkubwa kwa wake zao, watoto wao, dada zao,mama zao na ndugu zao wa kike. Kulingana na tamaduni zetu za kiafrika baba ndo mtafutaji na mwenyekauli ya mwisho katika familia" Alisema Dkt. Edna Nao wanafunzi wa shule ya msingi ya Bajavero walipata nafasi ya kuuliza maswali mbalimbali na kupata majibu pia kufurahishwa na elimu bora na kujitambua zaidi, pia walishukuru kupata zawadi za Pads aina ya Glory ikiwa ni kuelekea katika siku ya Hedhi duniani.

Thursday, 16 April 2015

KUELEKEA SIKU YA HEDHI DUNIANI, MTANDAO WA HEDHI SALAMA WAENDESHA SEMINA SHULE YA SEKONDARI ST. ANTHONY

 Kutoka kushoto ni Mkurugenzi mtendaji wa Kasole Secrets Hyasintha Ntuyeko ambao pia ni watengenezaji wa Pads za Glory, Katikati ni Mlezi wa wanafunzi Hilda Minja na Sara Mugele ambaye ni Dean of students  Shule ya Sekondari ya St. Anthony.
 Daktari Edna Kiogwe akieleza juu ya umuhimu wa elimu ya Hedhi kwa jamii nzima wakati wa semina na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya St. Anthony.
Mkurugenzi mtendaji wa Kasole Secrets Hyasintha Ntuyeko ambeye pia ni muandaaji wa siku ya Hedhi Duniani kwa Tanzania akielezea umuhimu wa kutunza Mazingira wanapokuwa Hedhi na kuithamini miundombinu.
 Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya St. Anthony wakiwa wanafuatilia kwa makini Semina hiyo.
 Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya St. Anthony wakifurahia Pads za Glory walizopewa ikiwa ni ishara ya kusherehekea sikukuu ya Hedhi Duniani.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya St.Anthony wakifurahia zawadi za Glory Pads baada ya Semina.