Monday, 12 December 2016

Ifakara yapata walimu 31 wa Hedhi Salama

 Jo Rees, nurse mbobezi katika elimu ya afya ya uzazi akiendesha mafunzo ya wakufunzi wa Hedhi Salama katika kijiji cha Ifakara kilichopo wilayani Kilombero mkoani Morogoro. Wakufunzi hawa ni wanafunzi wa masomo ya udaktari kutoka chuo cha Mt. Francis, ambao wanategemewa kufundisha kwa kujitolea katika shule za sekondari zilizopo Ifakara
 Jo Rees, akifundisha mbinu mbalimbali ambazo wakufunzi hawa wanatarajiwa kuzitumia katika kufundishia na hivyo kufanya darasa liwe na uhai na kila mmoja ajisikie huru kuchangia, ni muhimu kuendesha darasa hai, hasa pale unapokua unafundisha mada ambazo zinaonekana kutozungumzwa katika jamii
 Jo Rees, akielezea mfumo wa uzazi wa mwanamke
 Wakufunzi wakisikiliza kwa makini darasa lililokua linaendelea juu ya Hedhi Salama na Ukuaji na mbinu za kufikisha elimu hiyo kwa vijana wa shule za sekondari
 Mkufunzi Elikana akiuliza swali lake kuhusu nini anaweza kufanya endapo kijana shuleni atauliza swali linalohitaji majibu yasiyo wekwa wazi katika kadamnasi ya wanafunzi wengine
 Jo Rees akifundisha mbinu nyingine ambayo inaweza kuongeza uhai wa darasa na kuibua mijadala baina ya wanafunzi wenyewe. Mijadala hii inapaswa kusahihishwa na mkufunzi pale inapoelekea kwenye sintofahamu au kutoka nje kabisa ya agenda.
 Wakufunzi wakiibua mjadala juu ya mitazamo yao ya kile wanachokiamini, wakufunzi hawa walijigawa katika makundi mawili yenye kukubali au kutokubali jambo fulani lililowekwa mbele yao na hapo kila mmoja alitoa mtazamo wake uliomfanya kukubaliana au kutokubaliana na jambo fulani
 Jo Rees alifundisha pia mbinu nyingine ambayo itawasaidia wanafunzi katika kufanya maamuzi sahihi hasa pale wanapoamua kuanzisha mahusiano au katika kuchagua washauri
 Wakufunzi wakifuatilia kwa umakini maelekezo wanayopatiwa
 Mijadala ikiendelea katika makundi mbalimbali
Mmoja wa wakufunzi akielezea wenzake juu ya yale waliyoyachambua katika mjadala mdogo kundini kwake

 Jo Rees, alifundisha pia jinsi ya kuwafundisha vijana kupanga malengo, kuweka nia na kufikiria juu ya changamoto watakazotarajia kuzipitia na jinsi gani wanaweza kupambana na changamoto hizo ili kufikia malengo waliyojiwekea
 Michezo ni moja ya mbinu muhimu mno katika kufanikisha kuendesha darasa hai. Jo alifudisha michezo mbalimbali ambayo iliwafanya wakufunzi wote kushiriki bila kuchoka
Mtazamo na uelewa wa kila mmoja wetu juu ya jambo fulani unastahili kuheshimiwa na kusahihishwa kwa upendo kwa manufaa ya wote. Wakufunzi walipata nafasi ya kuelezea kile wanachokiamini kwa kuweka  maoni yao kwenye visanduku

Wakufunzi wakifanya mchezo mwingine wenye nia ya kujenga ujasiri pale unapoamua kufanya au kutokufanya jambo fulani, mchezo  huu humfanya mchezaji kua na jibu moja tuu lisilojichanganya na kutuma taarifa ya ndio wakati mchezaji alimaanisha hapana

Picha ya pamoja na wakufunzi wabobezi Jo Rees, Ivana Laic na wanafunzi  31 wa masomo ya udaktari katika chuo cha Mt. Francis ambao walipokea mafunzo ya Hedhi Salama chuoni hapo.Bi Hyasintha Ntuyeko, mkurugenzi mtendani wa Kasole Secrets aliungana na wakufunzi hawa wabobezi katika kufanikisha mafunzo haya.












0 comments: