Sunday, 4 September 2016

Walimu waunga mkono programu ya Hedhi Salama mashuleni mwao

 Mwalimu Prisca Mihayo, kutoka shule ya sekondari Meli iliyopo Moshi Vijijini akikagua kazi za vikundi walizopewa watoto katika kujadili ukuaji na mabadiliko mbalimbali yanayotokea katika mwili
 Mwalimu Prisca akifundisha mchezo ili kuwajengea wanafunzi uwezo na ujasiri wa kusoma pamoja kuhusu ukuaji na mabadiliko ya mwili
 Wanafunzi wakijadili kwa kina juu ya ukuaji na mabadiliko ya mwili katika vikundi vyao
Wanafunzi wakiwasilisha maoni yao kwa wanafunzi wenzao juu ya ukuaji na mabadiliko mbalimbali ya mwili baada ya kumaliza kazi za vikundi
 Wanafunzi wakifanya mchezo mwingine ujulikanao kama nyani, mchezo huu unawajengea wanafunzi uwezo wa kutafakari na kukubaliana pamoja baada ya kupima kwa kina matokeo ya maamuzi yao
 Bhavya Doshi, mwanafunzi wa udaktari kutoka KCMC amabaye pia ni mwalimu wa kujitolea akifundisha hedhi salama na ukuaji katika shule ya sekondari Meli, akiwafundisha wanafunzi mchezo mwingine
 Wanafunzi wakifanya kazi za vikundi
 Bhavya Doshi na wanafunzi wote kwa pamoja katika michezo, lengo ni kuwajengea ujasiri wanafunzi wa kike kwa wakiume kuvunja ukimya





0 comments: