Pongezi nyingi mno kwa wadau hawa ambao wameona uhitaji wa wanawake/mabinti hasa katika kuhakikisha wanaweza kujisitiri katika hali ya usafi na usalama wakati wowote na popote bila kudhalilika
Thursday, 21 April 2016
PAMOJA TANZANIA CLUBS WAAMUA KUONYESHA MFANO KWA WANAFUNZI WENZAO
12:16
No comments
Wanafunzi wa kiume waisafisha vyoo vyao, ikiwa ni moja ya shughuli zilizopangwa katika club ya Pamoja
Mwanafunzi wa kike katika Pamoja club akisafisha choo, ikiwa ni moja ya shughuli zilizopangwa ndani ya Pamoja club
Wanafunzi wote wakike kwa wakiume ndani ya Pamoja Club wakichota maji tayari kwa shughuli za usafi kuanza
Wanafunzi wa Pamoja Club wakinawa mikono mara baada ya zoezi la usafishaji choo kumalizika
Wanafunzi wote wa club ya Pamoja Tanzania, wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza zoezi la kusafisha choo, hongereni sana wakufunzi wetu, Lilian Benjamin (Hubert Kairuki) na Deusi Kapufi (KAM)
Friday, 26 February 2016
WANAFUNZI WAWA WALIMU WA WANAFUNZI WENZAO KUHUSU HEDHI SALAMA NA BALEHE-IFAKARA
14:38
No comments
Hili ni juma la 6 kati ya majuma 12 ambayo wanafunzi hawa wanatarajiwa kuhudhuria vipindi hivi vya hedhi salama na balehe, katika hili juma la 6 wanafunzi walifanya karakana ambapo waliwaalika wanafunzi wenzao ambao hawakupata nafasi ya kujiunga kwenye club, na badala yake hawa waliopata nafasi waliweza kuwafundisha wenzao yale yote waliyofundishwa ndani ya majuma 6 na kujibu maswali kwa usahihi kabisa bila uoga wala aibu, hii inaonyesha ni jinsi gani wanafunzi hawa wanavyoweza kua msaada kwa wanafunzi wenzao, ndugu na hata marafiki zao. Hongereni sana wafundishaji wetu wa kujitolea kutoka chuo cha Udaktari cha Mt. Francis-Ifakara
Tuesday, 23 February 2016
HEDHI SALAMA MOJA KATI YA PROGRAM BORA , ILIYOCHAGULIWA KUPELEKA MWAKILISHI MALTA-NETHERLANDS
08:58
No comments
Program ya hedhi salama ni moja kati ya program bora iliyochaguliwa kwenda kushiriki maonyesho yanayofanywa na Umoja wa wanafunzi wa vyuo vya udaktari duniani,( IFMSA) maonyesho haya yatafanyika Malta nchini Netherlands, hongera sana timu ya wanafunzi wa udaktari nchini Tanzania(TAMSA), kwa kujitolea kwa moyo na akili zote kuwafundisha wanafunzi kuhusiana na hedhi salama pamoja na balehe, Kazi yenu nzuri imezaa matunda, Kwa mujibu wa TAMSA hii ni mara yao ya kwanza kwenda katika Tamasha hili wakiwa na kazi ya kijamii ya kuonyesha.
Subscribe to:
Posts (Atom)
The Property of
Popular Posts
-
Miaka 7 iliyopita wakati Kasole Secrets wanaanzisha campaign za Hedhi Salama, ilionekana kama ni udhalilishaji kwa watoto wa kike na kina ...
-
Mwalimu Prisca Mihayo, kutoka shule ya sekondari Meli iliyopo Moshi Vijijini akikagua kazi za vikundi walizopewa watoto katika kujadili...
-
Jo Rees, nurse mbobezi katika elimu ya afya ya uzazi akiendesha mafunzo ya wakufunzi wa Hedhi Salama katika kijiji cha Ifakara kilichopo...
-
Kampuni ya Kasole Secrets imetambulisha program yake ya Pamoja club katika mashule, program hii inalenga kuwajengea uwezo , kuwapa nia ...
-
Kikundi cha ngoma kikitumbuiza katika sherehe za hedhi salama duniani, zilizofanyika Tanzania kwa mara ya kwanza ...
-
Kampuni ya Kasole secrets inayoendesha mtandao wa hedhi salama, leo wameendesha mafunzo ya hedhisalama na balehe kwa wanafunzi wana...
-
Katika mafunzo ya wakufunzi juu ya hedhi salama mradi unaofadhiliwa na ubalozi wa Marekani nchini Tanzania na kutekelezwa na Kampuni ya ...
-
Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wakifurahia vyeti vyao baada ya kufaulu vizuri mtihani wa hedhi salama na ukuaji uliopima uelew...
-
Dokta Aidat Mugula akizungumza na wanafunzi wa kiume walioonyesha shauku kubwa ya kutaka kuelewa zaidi juu ya maswala ya ukuaji B...
