Wednesday, 31 August 2016

Mkuu wa shule Benignis sekondari aomba mafunzo yawafikie wanafunzi wote shuleni hapo

Sr. Tryphonia Mgando, mkuu wa shule wa sekondari ya Benignis akifungua mahafali ya club ya Pamoja shuleni hapo
Wahitimu 40 wa Pamoja Club wakisimama kwa heshima na kuimba wimbo wa shule wakati wa mahafali ya club ya Pamoja katika shule ya wasichana Benignis
Wanafunzi waalikwa waliokuja kushuhudia wanafunzi wenzao wakihitimu mafunzo ya hedhi salama na ukuaji, wakiimba kwa heshima wimbo wa shule katika mahafali hayo
Wahitimu wa club ya Pamoja wakikabidhi risala yao kwa Mgeni Rasmi, Bi. Hyasintha Ntuyeko ,Mkurugenzi mtendaji wa Kasole Secrets
Wahitimu wakifanya igizo fupi juu ya balehe na changamoto wazipitiazo shuleni
Wahitimu wakiigiza tabia za watoto wa kiume wakifikia balehe na jinsi inavyokua hatari wakikosa washauri sahihi mapema
Sr. Tryphonia Mgando, akipokea cheti cha heshima kwa kuonyesha ushirikiano wa pekee katika kuhakikisha wanafunzi wake wanapatiwa muda wa kutosha kuhudhuria Club
Matroni shule ya sekondari Benignis akipokea cheti cha heshima
Mkuu wa Shule msaidizi, Mwl. Komba akipokea cheti cha heshima
Mwalimu wa taaluma, shule ya sekondari Benignis akipokea cheti cha heshima
Bwana. Revocutus Shigi akipokea cheti cha heshima kwa niaba ya umoja wa wanafunzi wa Udaktari Tanzania (TAMSA)
Wahitimu Pamoja Club, wakiwa katika picture ya Pamoja
Wanafunzi 40 katika shule ya Benignis walifanya mtihani na kufaulu vizuri na leo wamehitimu, tunategemea walimu hawa kua mfano na walimu wa wenzao hapo shuleni waliokosa nafasi ya kujiunga na club
Picha ya Pamoja kati ya wahitimu na jukwaa kuu baada ya kupokea vyeti vyao
Sr. Tryphonia Mgando akitoa shukrani zake za dhati kwa uongozi wa Kasole Secrets kwa kuwaletea program ya Pamoja shuleni kwake na kusaidia mabinti shuleni hapo, Sr. Tryphonia aliwaomba Kasole Secrets kuendelea na program hiyo hapo shuleni kwake ili wanafunzi wengi zaidi wafikiwe

Tuesday, 30 August 2016

WANAFUNZI 34 IFAKARA WAHITIMU MAFUNZO JUU YA HEDHI SALAMA NA UKUAJI

Wanafunzi Bravo sekondari wakifurahia vyeti vyao walivyotunukiwa baada ya kuhitimu mafunzo ya hedhi salama na ukuaji yaliyotolewa kwa muda wa wiki 12 shuleni hapo, Mafunzo haya yaliwaweka watoto wakike na wakiume katika club iliyopewa jina la Pamoja, Wanafunzi wa masomo ya udaktari kutoka chuo cha Mtakatifu Francis waliendesha mafunzo haya kwa wiki 12 chini ya usimamizi wa kampuni ya Kasole Secrets

Wahitimu wa Club ya Pamoja wakiimba wimbo katika mahafali yao ya hedhi salama na ukuaji
Wahitimu wa Pamoja Club, wakitoa igizo lao kuhusu hedhi salama na ukuaji, Igizo hili lilionyesha ni kwa kiasi gani mila na tamaduni zinavyoathiri vijana katika balehe
Timu nzima ya jukwaa kuu, ikichukua picture ya pamoja baada ya kumaliza zoezi zima la kugawa vyeti kwa wahitimu wa Pamoja Club
Mwalimu wa taaluma shuleni Bravo, Bwana Ally Msweta akikabidhiwa cheti cha heshima na Mkurugenzi mtendaji wa Kasole Secrets, Bi. Hyasintha Ntuyeko, ikiwa ni shukrani kwa kuonyesha ushirikiano wa pekee katika kuhakikisha wanafunzi wanapata muda wa kutosha katika kujifunza
Matroni Evodia akipokea cheti cha heshima baada ya kuonyesha ushirikiano wa pekee katika kuhakikisha wanafunzi wanahudhuria mafunzo kwa wakati
Bi. Regina Kway, akipokea cheti cha heshima kwa niaba ya Umoja wa wanafunzi madaktari Tanzania (TAMSA) kwa kukubali kujitoa kwao na kufundisha wanafunzi juu ya hedhisalama na ukuaji
Mwanafunzi Joshua Amani akipokea cheti chake baada ya kuhitimu mafunzo ya hedhi salama na ukuaji kwa majuma 12 shuleni Bravo
Mwanafunzi Mwanahamisi Juma, akipokea cheti chake cha uhitimu baaada ya kuhudhuria mafunzo kwa majuma 12 na kufaulu mtihani
Wahitimu wa Pamoja Club wakifuatilia kwa umakini ujumbe uliokua ukitolewa na daktari Elias kutoka hospitali ya Mt. Fransisco alipofika kwenye mahafali hayo
Daktari Elias, bingwa wa magonjwa ya kina mama kutoka hospitali ya Mt. Francis akiwapongeza wahitimu kwa kufuatilia vyema mafunzo juu ya hedhi salama na ukuaji yaliyotolewa shuleni hapo na kuwaambia kwamba anaamini mafunzo hayo yatawasaidia kujikinga na magonjwa
Mwalimu wa Taaluma shuleni Bravo, Bwana Alli Msweta akitoa tathimini ya uwepo wa Pamoja club shuleni hapo, Bwana Msweta alisema wanafunzi katika Club ya pamoja waliwasukuma kiasi wakaamua kuwajengea watoto wa kike tanuri la kuchomea taulo zilizotumika, Mwalimu Alli alisema pia Club hii imesaidia sana kubadilisha mienendo ya wanafunzi katika utunzaji wa mazingira na hata miili yao wenyewe

Thursday, 25 August 2016

WALIMU WATUNUKIWA VYETI HEDHI SALAMA

Baada ya kumaliza vyema mafunzo juu ya hedhi salama yaliyofanyika Moshi, Kasole Secrets Company Ltd na Msichana Initiative iliwatunuku vyeti vya uhitimu wakufunzi wote tayari kwa kwenda kufundisha watoto 500 wanaotegemewa kunufaika na mradi huu Moshi vijijini
 Afisa Elimu Afya na Lishe, Bi. Conjeta Kessy, akionesha cheti chake kwa furaha baada ya kuhudhuria kikamilifu mafunzo ya hedhi salama.
 Mwalimu Wilson Mrema kutoka Kidia secondary moja ya shule nufaika akipokea cheti chake baada ya kuhitimu mafunzo ya hedhi salama
 Mwalimu Prisca Mihayo kutoka Meli Secondary moja ya shule nufaika akipokea cheti chake baada ya kuhitimu mafunzo ya hedhi salama
 Mwalimu Anna Yohana kutoka shule ya msingi Mahoma moja ya shule nufaika akipokea cheti chake baada ya kuhitimu mafunzo ya hedhi salama

 Bwana Charles Mushi, mdau kutoka Shirika la Childreach akipokea cheti chake baada ya kuhitimu mafunzo ya hedhi salama
 Bi. Catherine Massawe, Mwanafunzi wa udaktari KCMC akipokea cheti chake baada ya kuhitimu mafunzo ya hedhi salama, Bi. Catherine anatarajiwa kwenda kufundisha Kidia Sekondari
 Bi. Harriet Sia mwanafunzi wa Udaktari KCMC akipokea cheti chake baada ya kuhitimu mafunzo ya hedhi salama, Bi. Harriet anatarajiwa kwenda kufundisha shule ya msingi Mahoma
Bwana. Ben Lepelali mwanafunzi wa udaktari KCMC akipokea cheti chake baada ya kuhitimu mafunzo ya hedhi salama, Bwana. Ben anatarajiwa kufundisha shule ya msingi Matemboni

WANAFUNZI WA MASOMO YA UDAKTARI WAFUNDISHWA KUTENGENEZA TAULO ZA KIKE

 Katika mafunzo ya wakufunzi juu ya hedhi salama mradi unaofadhiliwa na ubalozi wa Marekani nchini Tanzania na kutekelezwa na Kampuni ya Kasole Secrets na Msichana Initiative ambapo shule nne katika wilaya ya moshi vijijini ni wanufaika wa mradi huu. Wanafunzi wa masomo ya udaktari nane kutoka chuo cha udaktari KCMC na walimu wanne wa afya kutoka katika shule nufaika,walihudhuria mafunzo ya hedhi salama kwa siku tatu, moja ya warsha iliyofanyika katika siku hizi tatu za mafunzo ni kutengeneza taulo za kike, chupi, mifagio na dawa za kusafishia chooni kwa kutumia rasilimali zinazopatikana katika mazingira yao, wakufunzi hawa wanatarajiwa kwenda kuwafundisha jumla ya wanafunzi 500 kwa muda wa wiki 12 katika shule walizopangiwa  
Mkufunzi Judith Mlay ambaye ni Mhandisi Msaidizi katika idara ya Utafiti- Tanzania Engineering and Manufacturing organisation aliongoza mafunzo haya ya vitendo.
 Judith Mlay akitoa ufafanuzi wa kina kwa swali lililoulizwa na Florence Lyimo, mmoja wa wadau wa hedhi salama.
 Bi Judith Mlay, akionyesha jinsi ya kutengeneza kamba kwa kutumia majani ya migomba, Bi Judith alifafanua kua kamba hizi zinaweza kutumiwa kama nyenzo muhimu ya kusaidia kufunika mapipa ya takataka yaliyotengenezwa kienyeji.

Wakufunzi wakiweka vipimo sawa tayari kwa kutengeneza taulo za kike
 Bi. Hyasintha Ntuyeko ( Mkurugenzi Kasole Secrets) akisaidia kikundi kingine cha wakufunzi kuweka vipimo sawa, tayari kwa kuanza zoezi la kutengeneza taulo za kike
 Kazi ya ushonaji wa taulo za kike ikianza rasmi katika kikundi kimojawapo
 Zoezi la utengenezaji taulo za kike, lilikua na hatua mbalimbali zenye kushughulisha akili na kufurahisha, jambo lililowafanya wakufunzi wa kiume kufurahia sana zoezi hilo na hata kujaribu kubuni design nyingine, zoezi hili lilitupa mbinu mpya kabisa ambayo tunaahidi kuitumia ili kuweza kuwapata wakufunzi wa kiume kwa wingi zaidi na tunaamini tutafikia kipindi ambacho itakua ni kawaida kabisa kwa neno pedi/taulo za kike kutamkwa hadhari na jinsia zote bila kuona aibu.
 Mkufunzi Judith Mlay akionyesha hatua ya kwanza ya taulo ya kike iliyotengenezwa katika zoezi aliloliendesha
 Bi Judith Mlay akielekeza hatua ya pili katika kutengeneza taulo hii ya kike

Monday, 8 August 2016

HEDHI SALAMA TRAINING FOR TRAINERS IN MOSHI

  Volunteers wa hedhi salama wakifanya presentation juu ya mchango wa jamii katika kufanikisha hedhi salama kwa watoto wa kike, mjadala huu uliongozwa na Mwl. Yohana, Julius (KCMC), Hariet (KCMC) na Bi. Conjeta Kessy (Afisa Elimu afya na lishe- Moshi Vijijini)
Volunteers wa hedhi salama wakifanya presentation juu ya mila na tamaduni mbalimbali zinazosababisha watoto wa kike washindwe kumudu hedhi salama. Mjadala huu uliongozwa na Mwl. Prisca, Bhavya (KCMC) na Charles (Childreach)
Volunteers wa hedhi salama wakifanya presentation kuhusu njia mbalimbali zinazotumiwa na watoto wa kike katika kujisitiri wakati wa hedhi, mjadala huu uliongozwa na Mwl. Lucy, Angelina (KCMC) na Mwl. Mrema
Dr. Aidat Mugula ambaye pia ni mwalimu wa wakufunzi wa hedhi salama akifafanua kwa kina juu ya hatua mbalimbali za hedhi na mfumo mzima wa uzazi wa mwanamke.

Bi. Rebeca Gyumi, mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya Msichana Initiatitive ambao pia ni watekelezaji wa program ya hedhi salama katika shule za msingi akitoa semina jinsi ya kua mbunifu katika kuongoza vikundi vya wanafunzi  mara volunteers hawa watakapoenda kufundisha juu ya hedhi salama katika shule zao.
Bi. Hyasintha Ntuyeko akiendesha semina juu ya mbinu mbalimbali za kufundisha watoto wa kiume kuhusu ukuaji na hedhi salama bila kuwafanya vijana hao kujisikia kudhalilishwa
Wanafunzi wa shule faidika wa mradi wa hedhi salama na wanafunzi wa masomo ya udaktari wakiwa katika group discussion, moja ya mbinu ambazo wakufunzi hawa watapaswa kuzitumia katika shule zao wakifundisha juu ya hedhi salama na ukuaji

Wakufunzi wakiwa katika mijadala ambapo walipatiwa maswali na kuyajadili na baadae kufafanua walichokijadili katika kundi kubwa lenye wakufunzi wote
Wakufunzi wakiandika yale waliyoyajadili katika kikundi chao, tayari kwa kuwasilisha katika kundi kubwa la wakufunzi wote
Dokta Aidat Mugula akitoa muongozo kwa wakufunzi wakati wakijiandaa kumsikiliza Jo Rees, Muuguzi mkongwe kutoka Australia ambae pia ni mtungaji wa muongozo wa mafunzo ya hedhi salama na ukuaji, yanayotumika kufundishia wakufunzi hawa katika warsha hii
Michezo ya Pamoja iliyofanywa na wakufunzi kwa lengo la kuimarisha umoja na kuchangamsha akili na mwili
Bwana Wilson Bigambo, akifundisha wahitimu wenzake mchezo mwingine
Michezo ni sehemu kubwa ya mbinu hodari kabisa katika kuwafundisha watoto wa kike na wakiume juu ya hedhi salama na ukuaji
Jo Rees akijibu maswali mbalimbali yaliyokua yanaulizwa na wakufunzi ni jinsi gani wanaweza kuwahamasisha watoto wakike na wakiume kusoma kwa pamoja juu ya hedhi salama na ukuaji bila kuhisi kudhalilishwa
Moja ya kikundi kikiwasilisha maoni yao katika group kubwa la wakufunzi wote baada ya kujadiliana kama kikundi
Wakufunzi wakipata chakula cha pamoja wakati wa mapumziko
Mazungumzo na kutengeneza mtandao baina ya wakufunzi wakati wa chakula