Thursday, 25 August 2016

WALIMU WATUNUKIWA VYETI HEDHI SALAMA

Baada ya kumaliza vyema mafunzo juu ya hedhi salama yaliyofanyika Moshi, Kasole Secrets Company Ltd na Msichana Initiative iliwatunuku vyeti vya uhitimu wakufunzi wote tayari kwa kwenda kufundisha watoto 500 wanaotegemewa kunufaika na mradi huu Moshi vijijini
 Afisa Elimu Afya na Lishe, Bi. Conjeta Kessy, akionesha cheti chake kwa furaha baada ya kuhudhuria kikamilifu mafunzo ya hedhi salama.
 Mwalimu Wilson Mrema kutoka Kidia secondary moja ya shule nufaika akipokea cheti chake baada ya kuhitimu mafunzo ya hedhi salama
 Mwalimu Prisca Mihayo kutoka Meli Secondary moja ya shule nufaika akipokea cheti chake baada ya kuhitimu mafunzo ya hedhi salama
 Mwalimu Anna Yohana kutoka shule ya msingi Mahoma moja ya shule nufaika akipokea cheti chake baada ya kuhitimu mafunzo ya hedhi salama

 Bwana Charles Mushi, mdau kutoka Shirika la Childreach akipokea cheti chake baada ya kuhitimu mafunzo ya hedhi salama
 Bi. Catherine Massawe, Mwanafunzi wa udaktari KCMC akipokea cheti chake baada ya kuhitimu mafunzo ya hedhi salama, Bi. Catherine anatarajiwa kwenda kufundisha Kidia Sekondari
 Bi. Harriet Sia mwanafunzi wa Udaktari KCMC akipokea cheti chake baada ya kuhitimu mafunzo ya hedhi salama, Bi. Harriet anatarajiwa kwenda kufundisha shule ya msingi Mahoma
Bwana. Ben Lepelali mwanafunzi wa udaktari KCMC akipokea cheti chake baada ya kuhitimu mafunzo ya hedhi salama, Bwana. Ben anatarajiwa kufundisha shule ya msingi Matemboni

WANAFUNZI WA MASOMO YA UDAKTARI WAFUNDISHWA KUTENGENEZA TAULO ZA KIKE

 Katika mafunzo ya wakufunzi juu ya hedhi salama mradi unaofadhiliwa na ubalozi wa Marekani nchini Tanzania na kutekelezwa na Kampuni ya Kasole Secrets na Msichana Initiative ambapo shule nne katika wilaya ya moshi vijijini ni wanufaika wa mradi huu. Wanafunzi wa masomo ya udaktari nane kutoka chuo cha udaktari KCMC na walimu wanne wa afya kutoka katika shule nufaika,walihudhuria mafunzo ya hedhi salama kwa siku tatu, moja ya warsha iliyofanyika katika siku hizi tatu za mafunzo ni kutengeneza taulo za kike, chupi, mifagio na dawa za kusafishia chooni kwa kutumia rasilimali zinazopatikana katika mazingira yao, wakufunzi hawa wanatarajiwa kwenda kuwafundisha jumla ya wanafunzi 500 kwa muda wa wiki 12 katika shule walizopangiwa  
Mkufunzi Judith Mlay ambaye ni Mhandisi Msaidizi katika idara ya Utafiti- Tanzania Engineering and Manufacturing organisation aliongoza mafunzo haya ya vitendo.
 Judith Mlay akitoa ufafanuzi wa kina kwa swali lililoulizwa na Florence Lyimo, mmoja wa wadau wa hedhi salama.
 Bi Judith Mlay, akionyesha jinsi ya kutengeneza kamba kwa kutumia majani ya migomba, Bi Judith alifafanua kua kamba hizi zinaweza kutumiwa kama nyenzo muhimu ya kusaidia kufunika mapipa ya takataka yaliyotengenezwa kienyeji.

Wakufunzi wakiweka vipimo sawa tayari kwa kutengeneza taulo za kike
 Bi. Hyasintha Ntuyeko ( Mkurugenzi Kasole Secrets) akisaidia kikundi kingine cha wakufunzi kuweka vipimo sawa, tayari kwa kuanza zoezi la kutengeneza taulo za kike
 Kazi ya ushonaji wa taulo za kike ikianza rasmi katika kikundi kimojawapo
 Zoezi la utengenezaji taulo za kike, lilikua na hatua mbalimbali zenye kushughulisha akili na kufurahisha, jambo lililowafanya wakufunzi wa kiume kufurahia sana zoezi hilo na hata kujaribu kubuni design nyingine, zoezi hili lilitupa mbinu mpya kabisa ambayo tunaahidi kuitumia ili kuweza kuwapata wakufunzi wa kiume kwa wingi zaidi na tunaamini tutafikia kipindi ambacho itakua ni kawaida kabisa kwa neno pedi/taulo za kike kutamkwa hadhari na jinsia zote bila kuona aibu.
 Mkufunzi Judith Mlay akionyesha hatua ya kwanza ya taulo ya kike iliyotengenezwa katika zoezi aliloliendesha
 Bi Judith Mlay akielekeza hatua ya pili katika kutengeneza taulo hii ya kike

Monday, 8 August 2016

HEDHI SALAMA TRAINING FOR TRAINERS IN MOSHI

  Volunteers wa hedhi salama wakifanya presentation juu ya mchango wa jamii katika kufanikisha hedhi salama kwa watoto wa kike, mjadala huu uliongozwa na Mwl. Yohana, Julius (KCMC), Hariet (KCMC) na Bi. Conjeta Kessy (Afisa Elimu afya na lishe- Moshi Vijijini)
Volunteers wa hedhi salama wakifanya presentation juu ya mila na tamaduni mbalimbali zinazosababisha watoto wa kike washindwe kumudu hedhi salama. Mjadala huu uliongozwa na Mwl. Prisca, Bhavya (KCMC) na Charles (Childreach)
Volunteers wa hedhi salama wakifanya presentation kuhusu njia mbalimbali zinazotumiwa na watoto wa kike katika kujisitiri wakati wa hedhi, mjadala huu uliongozwa na Mwl. Lucy, Angelina (KCMC) na Mwl. Mrema
Dr. Aidat Mugula ambaye pia ni mwalimu wa wakufunzi wa hedhi salama akifafanua kwa kina juu ya hatua mbalimbali za hedhi na mfumo mzima wa uzazi wa mwanamke.

Bi. Rebeca Gyumi, mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya Msichana Initiatitive ambao pia ni watekelezaji wa program ya hedhi salama katika shule za msingi akitoa semina jinsi ya kua mbunifu katika kuongoza vikundi vya wanafunzi  mara volunteers hawa watakapoenda kufundisha juu ya hedhi salama katika shule zao.
Bi. Hyasintha Ntuyeko akiendesha semina juu ya mbinu mbalimbali za kufundisha watoto wa kiume kuhusu ukuaji na hedhi salama bila kuwafanya vijana hao kujisikia kudhalilishwa
Wanafunzi wa shule faidika wa mradi wa hedhi salama na wanafunzi wa masomo ya udaktari wakiwa katika group discussion, moja ya mbinu ambazo wakufunzi hawa watapaswa kuzitumia katika shule zao wakifundisha juu ya hedhi salama na ukuaji

Wakufunzi wakiwa katika mijadala ambapo walipatiwa maswali na kuyajadili na baadae kufafanua walichokijadili katika kundi kubwa lenye wakufunzi wote
Wakufunzi wakiandika yale waliyoyajadili katika kikundi chao, tayari kwa kuwasilisha katika kundi kubwa la wakufunzi wote
Dokta Aidat Mugula akitoa muongozo kwa wakufunzi wakati wakijiandaa kumsikiliza Jo Rees, Muuguzi mkongwe kutoka Australia ambae pia ni mtungaji wa muongozo wa mafunzo ya hedhi salama na ukuaji, yanayotumika kufundishia wakufunzi hawa katika warsha hii
Michezo ya Pamoja iliyofanywa na wakufunzi kwa lengo la kuimarisha umoja na kuchangamsha akili na mwili
Bwana Wilson Bigambo, akifundisha wahitimu wenzake mchezo mwingine
Michezo ni sehemu kubwa ya mbinu hodari kabisa katika kuwafundisha watoto wa kike na wakiume juu ya hedhi salama na ukuaji
Jo Rees akijibu maswali mbalimbali yaliyokua yanaulizwa na wakufunzi ni jinsi gani wanaweza kuwahamasisha watoto wakike na wakiume kusoma kwa pamoja juu ya hedhi salama na ukuaji bila kuhisi kudhalilishwa
Moja ya kikundi kikiwasilisha maoni yao katika group kubwa la wakufunzi wote baada ya kujadiliana kama kikundi
Wakufunzi wakipata chakula cha pamoja wakati wa mapumziko
Mazungumzo na kutengeneza mtandao baina ya wakufunzi wakati wa chakula

Tuesday, 2 August 2016

MKUTANO NA WADAU KATIKA MANISPAA YA MOSHI VIJIJINI

 Mkutano na wadau wa afya juu ya program ya hedhi salama katika manispaa ya moshi vijijini
 Wadau wa afya katika wilaya ya Moshi wakisikiliza kwa makini ufafanuzi wa program ya hedhi salama unaotegemewa kuanzishwa katika shule za msingi na sekondari zilizopo moshi vijijini
 Bi Hyasintha Ntuyeko akieleza kwa kina madhumuni ya programu hii ya hedhi salama katika wilaya ya moshi vijijini
 Dokta Wonanji ambaye pia ni mganga mkuu katika wilaya ya moshi vijijini akisikiliza ufafanuzi wa programu hiyo ya hedhi salama unaotarajiwa kuanzishwa katika wilaya yake
Mdau wa afya akiuliza swali la ufafanuzi kwa Bi. Hyasintha Ntuyeko kuhusu programu ya hedhi salama wilayani hapo
 Bi. Hyasintha Ntuyeko ambae pia ni mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Kasole secrets akiendelea kujibu na kufafanua zaidi jinsi wanavyotarajia kuendesha program hiyo ya hedhi salama katika wilaya ya moshi vijijini
 Mganga mkuu wa wilaya ya moshi vijijini, Daktari Wonanji akitoa tathimini yake kuhusu mradi wa hedhi salama unaotarajiwa kuanza wilayani kwake

 Bi. Hyasintha Ntuyeko akiendelea kufafanua na kuelezea zaidi kwanini mradi wa hedhi salama umelenga kuwahusisha wanafunzi wa masomo ya udaktari kutoka KCMC na kuendelea kuwatoa wasiwasi wadau hawa kwani pia walimu wa afya wa shule zote ambazo zinatarajiwa kufaidika na mradi watapewa mafunzo maalum ambayo yatawasaidia kuendeleza elimu hii ya hedhi salama hata baada ya wao kufunga mradi
 Daktari Wonanji, akiagiza kua mradi wa hedhi salama pia ufikirie kufikia shule nyingi zaidi wilayani moshi vijijini, kwani kuna vijiji ambavyo vimeathirika mno na mabinti hawaendi shule kabisa wakiwa katika hedhi, pia Dr. Wonanji alitoa wito kwa mradi wa hedhi salama kuona ni jinsi gani wataweza kuzifikia shule hizo katika vijiji tajwa hasa katika awamu hii ya kwanza ambapo mradi wa hedhi salama unatarajiwa kutekelezwa
Bi. Hyasintha Ntuyeko akisikiliza kwa makini maoni mbalimbali ya wadau wa afya. Mradi wa hedhi salama katika wilaya ya moshi vijijini utatekelezwa na taasisi mbili yaan Msichana Initiative ambao watatekeleza katika shue za msingi na Kasole secrets co. ltd ambao watatekeleza katika shule za sekondari, taasisi hizi mbili zinapokea ufadhili kutoka ubalozi wa Marekani nchini Tanzania