Tuesday, 12 December 2017

Ufunguzi wa kisima cha maji katika shule ya msingi King'ong'o waambatana na mafunzo ya Hedhi Salama

Saturday, 13 May 2017

Thursday, 11 May 2017

EATV media house yatumia siku ya wanawake duniani kusaidia mabinti katika kipindi cha Hedhi

Miaka 7 iliyopita wakati Kasole Secrets wanaanzisha campaign za Hedhi Salama, ilionekana kama ni udhalilishaji kwa watoto wa kike na kina mama kuzungumzia katika uwazi kusuhu Hedhi Salama jambo lililohitaji usiri mkubwa kulingana na mila na tamaduni za muafrika. Vyombo vya habari vyote nchini viligomea kabisa kuzungumzia kuhusu Hedhi Salama. Leo mwaka 2017 agenda ya Hedhi salama imechukua sura mpya na uzito wa pekee kwa jamii nzima ya kitanzania. Vyombo vya habari pia vimeweza kuvunja ukimya huu na kuongelea kwa wazi kabisa kuhusu Hedhi Salama. Tuna wapongeza kituo cha habari cha EATV kwa  kwenda mbali zaidi na kuamua kuchangisha pads kutoka kwa wanajamii kwa ajili ya mabinti wanaokosa fedha kwa ajili ya kununua vifaa hivi na kujisitiri hasa wanapokua shuleni.
Mjadala wa Hedhi Salama ukipewa tafakari zaidi juu ya changamoto mbalimbali zinazopitiwa na mabinti hasa wawapo shuleni. Wa mwisho Kulia ni Maza Senare, mkurugenzi wa Maznat Bridal, akifuatiwa na Joyce Kiria, mtangazaji na muandaaji wa kipindi EATV. Anae fuata ni Bi. Hyasintha Ntuyeko, mkurugenzi wa kampuni ya Kasole Secrets na wa mwisho kabisa ni Bi Irene, mtangazaji EATV.
 Picha ya pamoja, baada ya kumaliza mjadala wa Hedhi Salama uliohitimisha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani katika kituo cha habari cha EATV