Friday, 9 June 2017

Watoto wenye mahitaji maalumu waadhimisha siku ya Hedhi Salama


Wanafunzi kutoka shule ya msingi Jeshi la Wokovu wakiimba ngonjera; kueleza changamoto wanazozipitia kipindi cha hedhi. Wanafunzi hawa pia walitoa maoni juu ya nini kifanyike
 Wanafunzi Viziwi kutoka shule ya msingi Twiga wakifanya igizo kuelezea changamoto zinazowakuta wasichana katika kipindi cha hedhi hasa wanapokua shuleni
 Mwanafunzi wa kike kutoka shule ya msingi Twiga akizungumza juu ya nini kifanyike ili kuweza kuwasadia mabinti wenye mahitaji maalumu
 Mkalimani kutoka shule ya msingi Twiga akitafsiria wanafunzi kuhusu yanayoendelea katika maadhimisho hayo
 Wanafunzi kutoka shule ya msingi Twiga wakishangilia jambo
 Walimu kutoka shule ya msngi Toa Ngoma wakisalimu wageni waalikwa na wanafunzi
 Rhohin kutoka Dar-es-salaam rotaract club akiwasalimu wageni waalikwa na wanafunzi
 Dar-es-salaam Rotaract club of young professionals wakikabidhi pedi za dharura ambazo zitahifadhiwa shuleni kwa matumizi ya dharura kwa mabinti ili kupunguza mabinti hawa kukatiza masomo na kuamua kurudi nyumbani
 Mwalimu Rehema akitoa mkono wa shukrani baada ya kukabidhiwa zawadi hizo kwa ajili ya mabinti shuleni kwake
 Mgeni rasmi, Mzee Solomoni Mkonyi akishuhudia makabidhiano ya pedi za dharura kwa ajili ya shule
Ndugu mgeni rasmi; Mzee Mkonyi akimkabidhi Mwenyekiti wa chama cha wasioona Tanzania zawadi hizi za pedi za dharura kama ishara  ya kuonyesha mwanzo wa utekelezaji wa programu ya hedhi salama kwa mabinti waishio na ulemavu mbalimbali 
 Mzee Mkonyi akizungumza kwa niaba ya Afisa Elimu- mahitaji maalumu Temeke kuhusu umuhimu wa idara ya kitengo maalumu kuanza kuweka pedi za dharura kwenye bajeti yao ya kuomba vifaa vya kufundishia, ili bnti aweze kusoma kwa amani na kuzingatia masomo
Wageni waalikwa na walimu wakiwapongeza wanafunzi kwa kushiriki vyema na kuonyesha michezo mbalimbali katika maadhiisho ya siku ya hedhi salama

0 comments: