Tuesday, 8 November 2016

Mganga mkuu wa wilaya Moshi ahadi kuboresha Hedhi Salama wilayani kwake

 Mganga Mkuu wa wilaya ya Moshi- Dr. Wonanji akiongea katika sherehe za kuhitimisha program ya hedhi salama iliyotekelezwa katika shule nne Moshi-vijijini. Program hii ya hedhi salama ilidumu kwa miezi mitatu wilayani hapo ikitekelezwa na mashirika ya Kasole Secrets na Msichana Initiative kwa ufadhili wa ubalozi wa Marekani
Afisa Elimu Afya wa wilaya ya Moshi, Bi. Conjeta Kessy akizungumza  juu ya mikakati endelevu itakayofanya hamasa iliyoletwa na program ya hedhi salama izidi kudumu katika shule nufaika.

 Bi. Angelina Kahangwa, mmoja kati ya wanafunzi wa udaktari ambao walifundisha wanafunzi wa shule za sekondari na msingi wilayani Moshi katika program ya hedhi salama, akielezea changamoto na mafanikio waliyoyapata kwa kipindi chote walichokua wakitekeleza mradi
Bi. Hyasintha Ntuyeko, Mkurugenzi mtendaji wa Kasole Secrets, akiwaaga walimu na wanafunzi katika sherehe za kuhitimisha mradi wa hedhi salama uliokua wa mafanikio makubwa wilayani Moshi

Monday, 7 November 2016

Wahitimu wote wa Hedhi Salama watunukiwa vyeti

Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wakifurahia vyeti vyao baada ya kufaulu vizuri mtihani wa hedhi salama na ukuaji uliopima uelewa wao.                                  
Walimu wa shule zote nne nufaika na umoja wa wanafunzi wa udaktari Moshi, wakabidhiwa zawadi za heshima kwa mchango wao mkubwa katika kufanikisha program ya hedhi salama
Wanafunzi waliofaulu vizuri sana na kushika nafasi ya kwanza katika mtihani wa hedhi salama na ukuaji walizawadiwa mabegi ya shule
Wanafunzi waliofanya vizuri na kushika nafasi ya pili katika mtihani wa hedhi salama na ukuaji walizawadiwa madaftari ya shule, pencils na vifutio.
Mgeni rasmi Dr. Wonanji akimkabidhi mwanafunzi Nice Lyatuu zawadi ya begi la shule, baada ya mwanafunzi huyo kufanya vizuri katika mtihani wa hedhi salama na kushika nafasi ya kwanza
Dr. Wonanji akikabidhi vyeti kwa wanafunzi waliohitimu mafunzo ya hedhi salama na ukuaji

Wanafunzi wamuonyesha Mganga Mkuu wa wilaya, Dr. Wonanji jinsi ya kutengeneza dawa ya chooni

Mwanafunzi kutoka shule ya msingi Matemboni, akimuonyesha mganga mkuu wa wilaya ya Moshi, Dr. Wonanji, pamoja na jopo lake jinsi ya kutengeneza dawa ya kutengenezea choo kwa kutumia vumbi la mkaa, majivu na chumvi
Mwanafunzi Robert Shayo kutoka shule ya msingi Matemboni, akionyesha vipimo vya mikono, vinavyohitajika ili kuweza kuwianisha mchanganyiko wa dawa hiyo ya kusafishia choo.

Mwanafunzi Leah Tarimo, kutoka shule ya msingi matemboni akichanganya mchanganyiko huo uliokwisha pimwa vizuri na mwanafunzi mwenzake Robert, tayari kabisa kwa kuanza kutumika katika shughuli za usafi
Mwanafunzi Leah, akiwa ameshikilia fagio lake alilolitengeneza mwenyewe, tayari kabisa kuonyesha jinsi anavyoweza kutumia dawa hiyo kusafisha choo.
Mwanafunzi Robert, akionesha jinsi anavyoweza kutumia kibuyu chirizi kusafisha vizuri mikono yake mara baada ya kutoka chooni. Kibuyu hiki chirizi kimetengenezwa na wanafunzi wenyewe, ikiwa ni moja ya stadi walizofundishwa katika program ya hedhi salama shuleni hapo



Program ya Hedhi Salama Moshi vijijni imekua ya mafanikio makubwa

Wanafunzi wa kike kwa wakiume wakishirikiana kwa pamoja kutengeneza pedi ya kufua katika karakana waliyoifanya kama sehemu ya kuhitimisha mafunzo ya Hedhi Salama wilayani Moshi vijijini. Karakana hii ilikaguliwa na mgeni rasmi, Mganga Mkuu wa wilaya ya Moshi vijijini Dr. Vivian Wonanji
Wanafunzi wa kike kwa wakiume wakionyesha jinsi walivyoweza kujipatia maarifa ya kutengeneza chupi zao wenyewe
Vipimo mbalimbali na vifaa vya kutengenezea pedi za kufua vikiandaliwa na wanafunzi wote bila kujali jinsia, hatua hii imedhihirisha ni kwa kiasi gani programu ya Hedhi Salama iliweza kufanikiwa kuvunja ukimya.


Wanafunzi wahitimu wakionyesha ujuzi wao katika kutengeneza pedi za kufua
Kila mmoja alihakikisha anaelekeza watembeleaji na wanafunzi wenzao waliofika kutembelea karakana yao, jinsi ya kutengeneza pedi za kitambaa.
Binti kwa ushujaa kabisa akionesha pedi ya kitambaa aliyoitengeneza
Mganga Mkuu wa wilaya akitembelea karakana ya kutengeneza pedi za vitambaa na kuuliza maswali mbalimbali kwa wahitimu hawa.


                                         
 Wahitimu wakimuonyesha ndugu mgeni rasmi ambaye pia ni Mganga Mkuu wa wilaya jinsi wanavyoweza kutengeneza mafagio ya kusafishia vyoo kwa kutumia rasilimali zinazopatikana katika mazingira yao. Elimu hii imewatatulia changamoto ya kuacha vyoo vichafu kwa ajili ya ukosekanaji wa mafagio shuleni.                           
                                          
Wahitimu wakionyesha vifaa mbali mbali ambavyo vinaweza kutumika kama dustibini bila kuingia gharama yoyote.
                                           

Sunday, 6 November 2016

Wanafunzi Moshi vjijini wafanya mitihani kuhitimisha program ya Hedhi Salama

 Mradi wa hedhi salama katika wilaya ya Moshi vijijini umefikia tamati, wanafunzi wafanya mitihani kupima uelewa wa kile walichofundishwa kwa kipindi chote cha week 12. Mradi huu umetekelezwa na mashirika ya Kasole Secrets na Msichana Initiative kwa ufadhili wa ubalozi wa Marekani