Friday, 26 February 2016

WANAFUNZI WAWA WALIMU WA WANAFUNZI WENZAO KUHUSU HEDHI SALAMA NA BALEHE-IFAKARA

 Hili ni juma la 6 kati ya majuma 12 ambayo wanafunzi hawa wanatarajiwa kuhudhuria vipindi hivi vya hedhi salama na balehe, katika hili juma la 6 wanafunzi walifanya karakana ambapo waliwaalika wanafunzi wenzao ambao hawakupata nafasi ya kujiunga kwenye club, na badala yake hawa waliopata nafasi waliweza kuwafundisha wenzao yale yote waliyofundishwa ndani ya majuma 6 na kujibu maswali kwa usahihi kabisa bila uoga wala aibu, hii inaonyesha ni jinsi gani wanafunzi hawa wanavyoweza kua msaada kwa wanafunzi wenzao, ndugu na hata marafiki zao. Hongereni sana wafundishaji wetu wa kujitolea kutoka chuo cha Udaktari cha Mt. Francis-Ifakara






Tuesday, 23 February 2016

HEDHI SALAMA MOJA KATI YA PROGRAM BORA , ILIYOCHAGULIWA KUPELEKA MWAKILISHI MALTA-NETHERLANDS

Program ya hedhi salama ni moja kati ya program bora iliyochaguliwa kwenda kushiriki maonyesho yanayofanywa na Umoja wa wanafunzi wa vyuo vya udaktari duniani,( IFMSA) maonyesho haya yatafanyika Malta nchini Netherlands, hongera sana timu ya wanafunzi wa udaktari nchini Tanzania(TAMSA), kwa kujitolea kwa moyo na akili zote kuwafundisha wanafunzi kuhusiana na hedhi salama pamoja na balehe, Kazi yenu nzuri imezaa matunda, Kwa mujibu wa TAMSA hii ni mara yao ya kwanza kwenda katika Tamasha hili wakiwa na kazi ya kijamii ya kuonyesha.

Friday, 12 February 2016

SHULE ZA WAKIMBIZI ZAPATA FURSA YA KUELIMISHWA JUU YA HEDHI SALAMA

Bi. Hyasintha Ntuyeko akizungumza na mabinti katika moja ya shule ya secondary kambini Nyarugusu juu ya hedhi salama na balehe.
Mabinti wakitoa michango yao juu ya uelewa wao kuhusu balehe na hedhi salama na pia waliweza kuzungumzia juu ya njia mbalimbali wanazozitumia katika kujisitiri na hedhi wakiwa shuleni
Bi. Hyasintha Ntuyeko akisikiliza mijadala ya hedhi salama, iliyokua inafanywa na mabinti katika vikundi vidogo vidogo
Mama Letcia Lyogello akisimamia mijadala midigo midogo katika vikundi iliyokua inafanywa na mabinti shuleni hapo juu ya hedhi salama


Wanafunzi wa kike wakifanya kazi kwa Pamoja katika Vikundi
Wanafunzi wakiwakilisha mijadala yao, baada ya kumaliza kujadiliana katika vikundi walivyokua wamepangwa
Picha ya pamoja na wanafunzi baada ya kumaliza semina ya hedhi salama



WAKIMBIZI KAMBI YA NYARUGUSU WAPATA FURSA YA KUONGELEA JUU YA HEDHI SALAMA

Mmoja wa wakimbizi kutoka Congo akielezea baadhi ya mila zinazofuatiliwa na jamii kwa mwanamke anapokua hedhi                                   
Bi. Letisia Lyogello, muhamasishaji wa afya kambini  Nyarugusu kutoka shirika la TWESA, akielezea jinsi mtoto wa kike anavyoathirika na mazingira/miundo mbinu mibovu na hivyo kushidwa kujisitiri kabisa anapokua hedhi
Bi. Abilola Angelique ambaye pia ni mkimbizi kutoka Congo akielezea changamoto mbalimbali zinazomkumba mwanamke na binti kambini hapo na hivyo kushindwa kabisa kujisitiri wanapokua hedhi
Bi. Hyasintha Ntuyeko akizungumza na wafanyakazi kutoka mashirika mbalimbali na viongozi wa wakimbizi kambini Nyarugusu wilayani Kasulu kuhusu hedhi salama kua ni swala mtambuka, madhara yake hayaishii kwa mwanamke mtu bali jamii nzima

Bi. Elizabeth Morrissey, kutoka UNHCR akizungumzia umuhimu wa hedhi salama katika nyanja zote

Bwana Elia Sabula kutoka Shirika la Plan International akielezea umuhimu wa kuhusisha wanaume/wavulana ili kuweza kufanikisha hedhi salama katika nyanja zote za kijamii

Bwana George Tibaijuka kutoka UNHCR, akizungumzia juu ya hatua mbalimbali ambazo UNHCR inachukua katika kuhakikisha wanawake na mabinti wanaweza kujisitiri kambini hapo

Dr. Victor Nyange kutoka UNFPA akizungumzia madhara mbalimbali ya kiafya ambayo yanaweza kumkumba mwanamke endapo hata zingatia hedhi salama

Bi. Christina Mwita, kutoka shirika la IRC (International Refugees Committee) akielezea umuhimu wa kua na miundo mbinu yenye kumsitiri mwanake wakati wa hedhi katika vituo vyote vya kukusanyia wakimbizi (entry points)
Bi. Kimberly Height kutoka shirika la TWESA akizungumzia miundo mbinu ya vifaa vya maji na usafi wa mazingira na vifaa mbali mbali vinavyotumika na mwanamke wakati wa hedhi, Bi. Kimberly alieleza kua wanazingatia ujenzi wa vyoo ambavyo vitamsitiri binti/mwanamke wakati wa hedhi
UNHCR, wakionyesha vifaa vipya ambavyo wanatarajia kuanza kuwagawia wanawake na mabinti kwa ajili ya kuweza kujisitiri wakati wa hedhi na kuacha kutoa khanga ambazo walikua wakizigawa kwa wanawake/mabinti kwa matumizi ya hedhi, UNHCR walifafanua kua, wataendelea kutoa khanga kwa wanawake/mabinti kwa nia ya matumizi mbalimbali na si kwa ajili ya hedhi kama ilivyokua awali


Picha ya pamoja na wote waliohudhuria warsha ya hedhi salama kambini Nyarugusu