Jo Rees, nurse mbobezi katika elimu ya afya ya uzazi akiendesha mafunzo ya wakufunzi wa Hedhi Salama katika kijiji cha Ifakara kilichopo wilayani Kilombero mkoani Morogoro. Wakufunzi hawa ni wanafunzi wa masomo ya udaktari kutoka chuo cha Mt. Francis, ambao wanategemewa kufundisha kwa kujitolea katika shule za sekondari zilizopo Ifakara
Jo Rees, akifundisha mbinu mbalimbali ambazo wakufunzi hawa wanatarajiwa kuzitumia katika kufundishia na hivyo kufanya darasa liwe na uhai na kila mmoja ajisikie huru kuchangia, ni muhimu kuendesha darasa hai, hasa pale unapokua unafundisha mada ambazo zinaonekana kutozungumzwa katika jamii
Jo Rees, akielezea mfumo wa uzazi wa mwanamke
Wakufunzi wakisikiliza kwa makini darasa lililokua linaendelea juu ya Hedhi Salama na Ukuaji na mbinu za kufikisha elimu hiyo kwa vijana wa shule za sekondari
Mkufunzi Elikana akiuliza swali lake kuhusu nini anaweza kufanya endapo kijana shuleni atauliza swali linalohitaji majibu yasiyo wekwa wazi katika kadamnasi ya wanafunzi wengine
Jo Rees akifundisha mbinu nyingine ambayo inaweza kuongeza uhai wa darasa na kuibua mijadala baina ya wanafunzi wenyewe. Mijadala hii inapaswa kusahihishwa na mkufunzi pale inapoelekea kwenye sintofahamu au kutoka nje kabisa ya agenda.
Wakufunzi wakiibua mjadala juu ya mitazamo yao ya kile wanachokiamini, wakufunzi hawa walijigawa katika makundi mawili yenye kukubali au kutokubali jambo fulani lililowekwa mbele yao na hapo kila mmoja alitoa mtazamo wake uliomfanya kukubaliana au kutokubaliana na jambo fulani
Jo Rees alifundisha pia mbinu nyingine ambayo itawasaidia wanafunzi katika kufanya maamuzi sahihi hasa pale wanapoamua kuanzisha mahusiano au katika kuchagua washauri
Wakufunzi wakifuatilia kwa umakini maelekezo wanayopatiwa
Mijadala ikiendelea katika makundi mbalimbali
Jo Rees, alifundisha pia jinsi ya kuwafundisha vijana kupanga malengo, kuweka nia na kufikiria juu ya changamoto watakazotarajia kuzipitia na jinsi gani wanaweza kupambana na changamoto hizo ili kufikia malengo waliyojiwekea
Michezo ni moja ya mbinu muhimu mno katika kufanikisha kuendesha darasa hai. Jo alifudisha michezo mbalimbali ambayo iliwafanya wakufunzi wote kushiriki bila kuchoka