Sunday, 4 September 2016

Wanafunzi wafanya shughuli mbalimbali ikiwemo kusafisha vyoo

Wanafunzi wa kike wakichota maji tayari kwa kuanza zoezi la usafi wa choo, ambalo ni moja kati ya zoezi muhimu katika mtaala wa hedhi salama shuleni hapo
Mwalimu akitoa ufafanuzi kwa wanafunzi kuhusu workshop ya kusafisha choo inayofanyika shuleni hapo moja ya mada muhimu katika mtaala wa hedhi salama
Ben Lepilali, mkufunzi wa Hedhi salama kutoka KCMC, akiwaandaa wanafunzi wake katika shule ya matemboni kwa zoezi zima la kusafisha vyoo shuleni hapo
Mkufunzi Ben akiwaonyesha wanafunzi jinsi ya kusafisha vyoo
Mkufunzi Ben akiwagawia wanafunzi zawadi baada ya kushiriki vyema katika zoezi la kusafisha vyoo
Lineth Masala, project manager kutoka taasis ya Msichana Initiative ambao pia ni watekelezaji wa mradi wa hedhi salama katika shule za msingi wilayani Moshi vijijini akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi baada ya kumaliza zoezi la kusafisha vyoo
Mkufunzi Bhavya, kutoka KCMC akiwafundisha wanafunzi jinsi ya kutengeneza maumbo mbalimbali na kuandika majina yao katika maumbo hayo kama utambulisho wakati wakijiandaa na zoezi la kusafisha vyoo shuleni hapo
Wanafunzi Meli Sekondari wakivalishana majina yao yaliyoandikwa kwenye maumbo mbalimbali waliyoyatengeneza tayari kwa kuanza zoezi la usafishaji vyoo
Wanafunzi wakitengeneza wenyewe maumbo mbalimbali tayari kwa kuandika majina yao na kufanya usafi vyooni
Asia John mwakilishi wa kampuni ya Kasole Secrets ambao pia ni watekelezaji wa mradi wa hedhi salama katika shule za sekondari moshi vijijini akiwaonyesha wanafunzi mfano wa sabuni ya asili ya kusafishia vyoo, zoezi ambalo kila kikundi cha wanafunzi walilifanya

0 comments: