Tuesday, 26 July 2016

WANAFUNZI TAMSA WAFANYIWA USAHILI KUENDESHA HEDHI SALAMA CAMPAING












Mradi wa hedhi salama umepata ufadhili wa kuweza kufanyika katika shule nne ( 2- za msingi na 2 za sekondary) katika wilaya ya moshi vijijini, mradi huu ni wa pamoja katika utekelezaji ambapo katika shule za sekondary utasimamiwa na company ya Kasole secrets na katika shule za msingi shirika la Msichana Initiative litasimamia . Mradi huu unalenga kuwawezesha pia wanajumuiya/wanajamii wa Moshi kwa kuwapatia ujuzi wa kuendesha program hii ya hedhi salama hata baada ya muda wa ufadhili kuisha, hivyo tunatarajia kutrain wanafunzi wa masomo ya udaktari kutoka KCMC-Moshi ( TAMSA), Walimu wanne kutoka katika shule faidika na afisa mratibu wa afya shuleni.

Monday, 25 July 2016

MUONGOZO WA KUFUNDISHIA HEDHI SALAMA WATUMIKA MOSHI PIA

Muongozo wa mafunzo juu ya hedhi salama na ukuaji sasa umeongeza wigo kwa kutumika pia Moshi, mbali na hapo awali ulipokua ukitumika Dar-es-salaam na Ifakara. Muongozo huu ambao umeandiwa na muuguzi Jo Rees na kuweza kufanya vizuri sana katika shule za msingi na za sekondary nchini Ethiopia, kampuni ya Kasole secrets iliona ni vyema kuutumia pia muongozo huo katika program zao za hedhi salama nchini Tanzania. Bi Hyasintha Ntuyeko anasema ni mwaka sasa tangu waanze kuutumia muongozo huo, ambao ulitokea kupendwa sana na wanafunzi na walimu pia. Sasa muongozo huo utatumiwa tena kufundishia shule za moshi vijijini ambapo shirika la Msichana Inititive, Childreach na Tuleane watafundishwa jinsi ya kuutumia muongozo huu.

Wednesday, 20 July 2016

WSSCC NATIONAL CONSULTATION MEETING IN TANZANIA

WATER SUPPLY & SANITATION COLLABORATION COUNCIL (WSSCC) yawakutanisha wadau mbalimbali nchini Tanzania kujadili changamoto mbalimbli zinazoikumba nchi katika sector ya maji, sanitation and hygiene. Mdahalo huu uliwahusisha pia wadau kutoka Wizara ya maji, wizara ya afya, wizara ya elimu na TAMISEMI. Warsha hii ilitoa muelekeo wa pamoja kwa wadau na serikali katika kufanikisha tunatekeleza Suistanable Development Goal (SDG)