Sunday, 7 June 2015

SHEREHE ZA HEDHI SALAMA DUNIANI, ZAPAMBWA NA BURUDANI MBALIMBALI NCHINI TANZANIA, 28 MEI 2015




 Kikundi cha ngoma kikitumbuiza katika sherehe za hedhi salama duniani, zilizofanyika Tanzania kwa mara ya kwanza







 Mabinti kutoka New Hope for girls wakiimba wimbo uliobeba ujumbe mahususi kwa mwaka 2015, katika sherehe hizi za hedhi salama duniani zilizofanyika kwa mara ya kwanza nchini Tanzania
Picha ya pamoja

TANZANIA YAADHIMISHA SIKU YA HEDHI SALAMA DUNIANI, 28TH MAY 2015


 Wanafunzi na washiriki wengine wakiwa wamekusanyika Wizara ya Elimu tayari kwa kusubiri kuanza maandamano jijini Dar-es-salaam

 Band ya police ikiyapamba maandamano hayo ya siku ya hedhi salama, yaliyofanyika jijini Dar-es-salaam, 28th Mei 2015
 Waudhuriaji mbalimbali waliokuja kuadhimisha siku ya hedhi salama duniani
 Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Kasole Secrets, ambao pia ni waandaaji wa siku hii ya hedhi salama duniani, akiwashukuru wadau mbalimbali ambao walifanikisha siku hii kuadhimishwa kitaifa, alitoa shukrani zake kwa WIZARA YA ELIMU, WIZARA YA AFYA, WATER AID, SNV, UNICEF, ACCRACS, WSSCCS, SAWA, HELP TO KIDS, JHM & PPF
 Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Kasole Secrets Bi. Hyasintha Ntuyeko akikabidhi zawadi kwa Mheshimiwa Mgeni Rasmi, kutoka Wizara ya Elimu, Mama Madina Kemilembe
  Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Kasole Secrets Bi. Hyasintha Ntuyeko akikabidhi zawadi kwa Mheshimiwa mwakilishi wa NGOs zote zilizoshiriki katika kufanikisha tukio hili, kutoka Water aid (Country Director), Dr. Ibrahimu Kabole

 Kampuni ya TanManagement Insurance brokers ilidhamini Glory pads kugawiwa bure kwa wanafunzi wote waliohudhuria ikiwa ni moja ya kufanikisha sherehe hizi za hedhi salama Tanzania




 Makampuni na Mashirika mbalimbali yakionyesha bidhaa zao na kazi mbalimbali wanazofanya, katika viwanja vya mnazi mmoja katika maadhimisho ya siku ya hedhi duniani

 Kauli Mbiu ya mwaka 2015
Wanafunzi wakiendelea kugawiwa Glory pads ikiwa ni moja ya kusherehekea siku ya hedhi duniani

Saturday, 23 May 2015

TAARIFA RASMI KWA UMMA KUPITIA VYOMBO VYA HABARI

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kasole Secrets, na waandaaji wa siku ya hedhi duniani, Hyasintha Ntuyeko, akifungua mkutano na waandishi wa habari, tar 21 May 2015, katika ukumbi wa wizara ya afya.
                                       
     Msemaji wa Serikali Bibi Theresia Kuwite kutoka wizara ya elimu akifafanua zaidi kuhusu siku ya hedhi duniani, inayotarajiwa kufanyika tar 28 May mwaka huu, kwa mara ya kwanza, maandamano yataanzia Wizara ya Elimu saa mbili kamili asubuhi, na yanatariwa kuongozwa na Mheshimiwa naibu waziri wa Elimu, Mama Anna Malecela Kilango, pembeni ni msemaji kutoka shirika la Water aid, akiwakilisha mashirika yote ambayo yameshiriki katika kufanikisha sherehe hizi,mashirika hayo ni UNICEF, SNV, ACCRACC, WSSCC, WATER AID, SAWA, JHM & HELP TO KIDS
 Picha ya pamoja baada ya mjadala huo kumalizika.

Friday, 1 May 2015

MABINTI WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU, WAPATA NAFASI YA KUJIFUNZA JUU YA HEDHI SALAMA

 Binti wa Kijita akielezea mila za wajita kwa binti/mama aliyepohedhi, kua si ruhusa kuonana na baba yako, na unapaswa kukaa ndani huku ukiwa umevaa vazi moja la khanga tuu, mpaka hapo unapomaliza hedhi ndipo ubadilishe vazi hilo
Binti wa kichaga akielezea, jinsi alivyoogeshwa na magadi kwa nguvu, baada ya kuchuma maboga akiwa kwenye hedhi, anasema onyo hilo la kutokuchuma maboga alipewa na bibi yake mara tu alipoingia hedhi, lakini alilazimika kukiuka sharti hilo baada ya kuona amebaki mwenyewe nyumbani na usiku unaingia, hivyo alipaswa kuandaa chakula.
Binti wa Kisukuma akielezea siku ya kwanza alipovunja ungo, alimwambia mama yake, mama yake alimwambia kua asipike wala asiguse vyombo vyake mpaka hapo atakapomaliza, alisisitiza kua mama yake alimwambia shughuli hizo atazifanya tena, mara atakapohakikisha kua amemaliza siku zake.
Binti wa kichaga akielezea jinsi alivyokatazwa kuchuma dawa shambani na mama yake alipokua ameingia hedhi, anasema dada yake alimtuma akachume hiyo dawa shambani, anasema hakujua kama ni mwiko yeye kuichuma hiyo dawa, dada yake alijua kua ni mwiko ndo maana alimtuma yeye, lakini pia dada yake hakujua kama mdogo wake amevunja ungo na siku hiyo kua mdogo wake pia alikua katika siku zake.
 Wa kwanza kushoto ni bibi Consoler Elia, mlezi wa mabinti hawa, katikati ni Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Kasole Secrets, Hyasintha Ntuyeko, na wa tatu ni mtangazaji wa ITV, Blandina Sembu


Mabinti wakifurahia zawadi za Glory pads walizopatiwa na kampuni ya Kasole secrets katika maandalizi ya kujiandaa kusherehekea siku ya hedhi duniani, 28 May 2015