Saturday, 10 September 2016

Programu ya Hedhi Salama yafunguliwa rasmi- Moshi vijijini

 Wanafunzi wa shule ya Sekondari Meli wakisikiliza kwa makini ufunguzi wa program ya hedhi salama uliofanyika shuleni hapo
 Wanafunzi shule ya msingi Matemboni wakisikiliza kwa umakini ufunguzi wa programu ya hedhi salama
 Mwalimu mkuu shule ya secondari Meli akifungua rasmi program ya hedhi salama itakayofanyika katika shule nne, wilayani Moshi vijijini chini ya msaada wa ubalozi wa Marekeni nchini Tanzania
 Afisa Elimu, Moshi Vijijini, Bi. Conjeta Kessy akisisitiza umuhimu wa walimu wa afya katika shule hizi nne zitakazonufaika na mradi, kufuatilia programu hii ya hedhi salama kwa karibu, ili waweze kuindeleza vyema baada ya mradi kumalizika
Dr. Aidat Mugula, kutoka Kasole Secrets, ambae pia ni mfundishaji wa program ya hedhi salama kwa wanafunzi wa masomo ya udaktari nchini, akizungumza na wanafunzi wa shule za Matemboni na Meli katika ufunguzi wa programu shuleni hapo
 Rebeca Gyumi, Mkurugenzi wa taasisi ya Msichana Initiative, ambao pia ni watekelezaji wa programu ya hedhi salama katika shule za msingi Moshi vijijini akiongea na wanafunzi wa shule za Matemboni na Meli wakati wa ufunguzi

Picha ya pamoja na wazazi waliohudhuria ufunguzi wa programu ya hedhi salama
 Picture ya pamoja na baadhi ya wanafunzi katika ufunguzi wa programu ya hedhi salama moshi vijijini
Picture ya pamoja na walimu na volunteers kutoka KCMC katika sherehe za ufunguzi wa programu ya hedhi salama Moshi vijijini

Sunday, 4 September 2016

Wanafunzi wafanya shughuli mbalimbali ikiwemo kusafisha vyoo

Wanafunzi wa kike wakichota maji tayari kwa kuanza zoezi la usafi wa choo, ambalo ni moja kati ya zoezi muhimu katika mtaala wa hedhi salama shuleni hapo
Mwalimu akitoa ufafanuzi kwa wanafunzi kuhusu workshop ya kusafisha choo inayofanyika shuleni hapo moja ya mada muhimu katika mtaala wa hedhi salama
Ben Lepilali, mkufunzi wa Hedhi salama kutoka KCMC, akiwaandaa wanafunzi wake katika shule ya matemboni kwa zoezi zima la kusafisha vyoo shuleni hapo
Mkufunzi Ben akiwaonyesha wanafunzi jinsi ya kusafisha vyoo
Mkufunzi Ben akiwagawia wanafunzi zawadi baada ya kushiriki vyema katika zoezi la kusafisha vyoo
Lineth Masala, project manager kutoka taasis ya Msichana Initiative ambao pia ni watekelezaji wa mradi wa hedhi salama katika shule za msingi wilayani Moshi vijijini akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi baada ya kumaliza zoezi la kusafisha vyoo
Mkufunzi Bhavya, kutoka KCMC akiwafundisha wanafunzi jinsi ya kutengeneza maumbo mbalimbali na kuandika majina yao katika maumbo hayo kama utambulisho wakati wakijiandaa na zoezi la kusafisha vyoo shuleni hapo
Wanafunzi Meli Sekondari wakivalishana majina yao yaliyoandikwa kwenye maumbo mbalimbali waliyoyatengeneza tayari kwa kuanza zoezi la usafishaji vyoo
Wanafunzi wakitengeneza wenyewe maumbo mbalimbali tayari kwa kuandika majina yao na kufanya usafi vyooni
Asia John mwakilishi wa kampuni ya Kasole Secrets ambao pia ni watekelezaji wa mradi wa hedhi salama katika shule za sekondari moshi vijijini akiwaonyesha wanafunzi mfano wa sabuni ya asili ya kusafishia vyoo, zoezi ambalo kila kikundi cha wanafunzi walilifanya

Walimu waunga mkono programu ya Hedhi Salama mashuleni mwao

 Mwalimu Prisca Mihayo, kutoka shule ya sekondari Meli iliyopo Moshi Vijijini akikagua kazi za vikundi walizopewa watoto katika kujadili ukuaji na mabadiliko mbalimbali yanayotokea katika mwili
 Mwalimu Prisca akifundisha mchezo ili kuwajengea wanafunzi uwezo na ujasiri wa kusoma pamoja kuhusu ukuaji na mabadiliko ya mwili
 Wanafunzi wakijadili kwa kina juu ya ukuaji na mabadiliko ya mwili katika vikundi vyao
Wanafunzi wakiwasilisha maoni yao kwa wanafunzi wenzao juu ya ukuaji na mabadiliko mbalimbali ya mwili baada ya kumaliza kazi za vikundi
 Wanafunzi wakifanya mchezo mwingine ujulikanao kama nyani, mchezo huu unawajengea wanafunzi uwezo wa kutafakari na kukubaliana pamoja baada ya kupima kwa kina matokeo ya maamuzi yao
 Bhavya Doshi, mwanafunzi wa udaktari kutoka KCMC amabaye pia ni mwalimu wa kujitolea akifundisha hedhi salama na ukuaji katika shule ya sekondari Meli, akiwafundisha wanafunzi mchezo mwingine
 Wanafunzi wakifanya kazi za vikundi
 Bhavya Doshi na wanafunzi wote kwa pamoja katika michezo, lengo ni kuwajengea ujasiri wanafunzi wa kike kwa wakiume kuvunja ukimya