Mkurugenzi wa chuo cha Ualimu, bwana Justin Francis akimkaribisha mgeni rasmi Bi. Hyasintha Ntuyeko katika Mkutanano wa Kitaifa wa walimu, uliohudhuriwa na wawakilishi Tanzania nzima, Mkutano huu ulifanyika Bagamoyo, 16th June 2015
Bi Hyasintha Ntuyeko akiwasalimu walimu waliohudhuria katika mkutano mkuu wa Kitaifa wa walimu-Bagamoyo
Bi. Hyasintha Ntuyeko, akiongea na walimu juu ya hedhi salama.
Walimu wakisikiliza kwa makini juu ya hedhi salama.
Mada juu ya hedhi salama ilionekana kuwavutia sana walimu hawa na baadae kuzua mchango kutoka kwa washiriki hawa, walioleza changamoto zao wakiwa kama walimu na pia changamoto za wanafunzi wao.
Mgeni Rasmi Bi. Hyasintha Ntuyeko akiserebuka na walimu ikiwa ni makubaliano ya utekelezaji wa walimu hawa kuirithisha elimu ya hedhi salama waliyoipata kwa wanafunzi wao na familia zao.