Picha ya pamoja na wadau wote ambao walishiriki kuandaa siku ya hedhi salama duniani
Wadau katika jukwaa kuu
Mgeni Rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mh. Raymond Mushi, ambaye alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-salaam. Mhe. Raymond Mushi akizungumza na wananchi
Mwanafunzi Celina Fransis kutoka Manyara akiongelea hali halisi ilivyo katika kujihifadhi wakati wa hedhi katika shule za vijijini
Mwanafunzi kutoka shule ya Msingi Tandale akimsomea risala Muheshimiwa Mgeni Rasmi
Mjadala wa wazi, uliochambua kwa kina tatizo la hedhi salama nchini
Wadau wakionyesha, shughuli zao mbalimbali wanazozifanya
Rebeca Gyumi kutoka Msichana Initiative, akiongoza mjadala wa wazi uliofanywa na watafiti na wachambuzi mbali mbali
Wageni waalikwa na wanafunzi wakisikiliza kwa makini mdahalo wa wazi uliokua unaendelea katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar-es-salaam
Matembezi ya hiari yaliyoungwa mkono na watu mbalimbali akiwemo mwanamitindo maarufu mwenye jina kubwa duniani, Flaviana Matata, wasanii Mwasiti, Lina, Shilole na Queen Darlene, Pia Taasis ya Hassan Maajar
Watoto kutoka Hope for Girls wakiimba wimbo maalumu kwa ajili ya siku ya hedhi salama duniani
Wasanii Mwasiti, Queen Darlene na Shilole wakiimba katika sherehe za siku ya hedhi salama duniani
Bi. Hyasintha Ntuyeko, Mkurugenzi mtendaji Kasole Secrets Company, akiwashukuru wageni waalikwa, wadau wote waliofanikisha tukio hili muhimu la hedhi salama kufanyika tena nchini, Bi. Hyasintha aligawa zawadi kwa mgeni Rasmi, Mwakilishi ofisi ya Rais, wizara ya Elimu na Wizara ya afya kwa kuonyesha ushirikiano wa kifani katika kufanikisha siku ya hedhi salama duniani
Mgeni Rasmi, Mhe. Raymond Mushi, akipokea zawadi yake kutoka Kasole Secrets co.ltd
Dr. Hamisi Masanja Malebo, akipokea zawadi yake kwa niaba ya waziri wa Afya
Bwana Nehemia Mandia, akipokea zawadi yake kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Tanzania , Mhe. Mama Samia Suluhu
Mama Theresia Kuiwite kutoka Wizara ya Elimu, akimkabidhi mgeni rasmi kanga yenye ujumbe mahususi kama alama ya kumbukumbu katika kusaidia watoto wa kike katika kupata mazingira rafiki ambayo yatawafaa katika kipindi cha hedhi pia
Afisa Elimu wilaya ya Kinondoni, Bw. Rodgers Shemweleta, akisikiliza kwa makini Risala iliyokua inasomwa na wanafunzi
Pembeni ya Mgeni Rasmi, kulia ni Rebeca Budimu kutoka UNICEF na kushoto ni Bibi. Lilian Liundi, Mkurugenzi wa Tanzania Gender Network (TGNP)