Ni wazi kwamba Serikali yetu ipo macho na wadau wa maendeleo pia wapo macho, katika kuona ni jinsi gani watakaa pamoja na kutafuta suluhusho la kudumu kwa mabinti/wanawake ambao ni zaidi ya asilimia 50 ya Watanzania wote.
Karibuni wote katika mtembezi ya hiari yanayotarajiwa kuanza wizara ya Elimu saa mbili kamili asubuhi, kuelekea viwanja vya mnazi mmoja, Mgeni Rasmi anatarajiwa kua Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-salaam anaetarajiwa kumuwakilisha Muheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Hassani Suluhu