Friday, 16 October 2015

UTAMBULISHO WA PAMOJA CLUBS KATIKA SHULE ZA SECONDARY WAANZA RASMI

 Kampuni ya Kasole Secrets imetambulisha program yake ya Pamoja club katika mashule, program hii inalenga kuwajengea uwezo , kuwapa nia ya kuthubutu na kuweka tofauti katika ufikiriaji na utendaji, wanafunzi wa kike kwa wakiume, Kiini cha clubs hizi ni uhamasishaji wa hedhi salama mashuleni


 Program hii ya Pamoja club imepokelewa kwa hamasa na nguvu kubwa na wanafunzi wote wa kike kwa wakiume

Wanafunzi wakiandikisha majina yao, tayari kwa kuhudhuria Pamoja club


Tuesday, 13 October 2015

MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA KIKE DUNIANI-KONDO SECONDARY

Wanafunzi wa kike na wakiume wa shule ya secondary Kondo walipata fursa ya kusherehekea siku ya mtoto wa kike duniani- program hii iliandaliwa na ubalozi wa Marekani kupitia program yao ya Access
Mkurugenzi wa Kampuni ya Kasole secrets Bi. Hyasintha Ntuyeko akiwa pamoja na wanafunzi katika kikundi waliokua wakijadili matatizo yanayomkabili binti wa Kitanzania 
Wanafunzi wa kike walipata pia nafasi ya kujadili changamoto mbalimbali zinazowakumba katika kukabiliana na hedhi salama
Bi. Hyasintha Ntuyeko, aliwapatia mabinti hawa zawadi ya taulo za Glory ikiwa ni ishara ya kusherehekea siku ya mtoto wa kike Duniani

MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA KIKE DUNIANI- KAMBANGWA SECONDARY SCHOOL
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Kasole Secrets, Bi. Hyasintha Ntuyeko akizungumza na wanafunzi wa secondary ya Kambangwa katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani- program hii iliandaliwa na ubalozi wa Marekani kupitia program yao ya Access
 Wanafunzi wakisikiliza kwa makini
 Mijadala mbalimbali juu ya changamoto za mtoto wa kike, ilifanywa kwa pamoja na wanafunzi katika vikundi tofauti
 Wanafunzi wakiwasilisha mchango wao kuhusu changamoto zimpatazo mtoto wa kike
Kundi lingine likiwasilisha maoni yao juu ya nini kifanyike ili kumkwamua mtoto wa kike
 Palikua na mjadala mwingine wa watoto wa kike tuu na walimu wao, juu ya changamoto zinazohusiana na hedhi salama na hasa inavyowaathiri watoto hawa wakike katika mahundurio yao ya darasani
Mkurugenzi wa Kampuni ya Kasole Secrets, Bi. Hyasintha Ntuyeko aliwapatia mabinti hawa taulo za Glory ikiwa ni ishara ya kusherehekea siku ya mtoto wa kike duniani, Kulia mwisho ni Bi. Merisa kutoka Ubalozi wa Marekani